English Kona

Hot

Post Top Ad

LightBlog

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, 20 June 2019

"My" au "Mine" ? - Jifunze kutofautisha.

02:53 0Katika grammar ya kiingereza tuna possessive adjectives na possessives nouns.

Possessive adjectives - Vivumishi vya umiliki.
( My , your , his , her , its , our  , their )

Possessive pronouns - Viwakilishi vya umiliki.
( Mine, yours , his , hers , its, ours , theirs )

Tunatumia maneno haya kuelezea au kutaja vitu ambavyo tunavimiliki. Sasa leo tujifunze ni wakati gani wa kutumia maneno haya kwa ufasaha. Baada ya kusoma somo hili basi utaweza kuyatumia maneno haya kwa usahihi.

Tumia  "MY" kabla ya jina au majina ya vitu tunavyomiliki na tumia  "MINE" baada ya jina au majina ya vitu tunavyomiliki.


* Anna is my friend.
(Anna ni rafiki yangu.)

* Anna is a friend of mine.
(Anna ni rafiki yangu.)

* Those are  my glasses.
( Hayo ni miwani yangu.)

* Those glasses are mine.
(Mawani hayo ni yangu.)

* This is my dog.
( Huyu ni mbwa wangu.)

* This dog is mine.
( Mbwa huyu ni wangu.)

* Your dog is bad. Mine is good.
( Mtoto wako ni mbaya. Wangu ni mzuri )

* This cat is mine not yours.
(Huyu paka ni wangu na sio wako.)


TUANGALIE MIFANO YA JUMLA YA POSSESSIVE ADJECTIVES NA POSSESSIVE PRONOUNS 👇👇👇

 MIFANO ZAIDI

1. This is his car. This car is his.
- Hili ni gari lake. Gari hili ni lake.

2. This is her ring. This ring is hers.
 - Hii ni pete yake. Pete hii ni yake.
( SIO : This ring is her. )

3. This is their radio. This radio is theirs.
- Hii ni radio yao. Redio hii ni yao.
( SIO : This radio is their. )

Jifunze pia jinsi ya kutofautisha kati ya "I" na "Me" 👇👇👇

Tazama hapa chini 👇👇👇


Unataka kuongea kiingereza kwa ufasaha ? Bofya hapa kujua zaidi => ENGLISH COURSE
Tufuatile :

Facebook, twitter na Instagram kwa jina la English Kona.

Read More

Sunday, 16 June 2019

VIDEO : Jifunze tofauti kati ya "I" na "Me"

13:42 0
Watu wengi wanaojifunza kiingereza huchanganya matumizi kati ya "I" na "Me" hasa hasa pale wanapoyatumia pamoja na majina ( noun ).

Katika video hii 👇👇👇  utajifunza jinsi ya kutofautisha na kuyatumia maneno haya kwa usahihi kabisa.

Watch video 👇👇👇

Read More

Saturday, 8 June 2019

Jinsi ya kusoma saa kwa kiingereza. ( Time telling )

07:45 0


Karibu tena English Kona kujifunza mawili matatu katika lugha ya kiingereza. Katika somo letu la leo tutajifunza jinsi ya kusoma na kutaja muda katika lugha ya kiingereza.

Kabla hatujaendelea , tujikumbushe hili usomaji wa saa za kiingereza ni tofaut na kiswahili ... Kwa mfano ikiwa 7 kwa kiswahili tunasema moja.

 _Angalia vizuri hapa_ :

1 = 7
2 = 8
3 = 9
4 = 10
5 = 11
6 = 12
7 = 1
8 =  2
9  =  3
10 = 4
11 = 5
12 = 6

Lakini katika kiingereza huwa tunataja namba kama zilivyo.

 JINSI YA KUTAJA NA KUSOMA MUDA.

Kuna njia mbili za kutaja mda

1. Kuanza kutaja saa kwanza alaf dakika. ( Hour + Minutes )

* 6:25 - It's six twenty-five.
- Ni saa kumi na mbili na dakika ishirini na tano.

* 9:05 - It's nine O-five ( O inatamkwa kama herufi O )
- Ni saa tatu na dakika  tano.

* 9:11 - It's nine eleven.
- Ni saa tatu na dakika kumi na moja.

2. Kutaja dakika kwanza alafu saa.
( Minutes + PAST / TO + Hour )

Kwa dakika 1-30 tunatumia PAST baada ya kutaja dakika.

Kwa dakika 31-59 tunatumia  TO baada ya kutaja dakika.

 _FAHAMU HILI_ :

Tunapotumia TO ina maana tunazungumzia kasoro. Sasa kwa mfano :

12 : 40 - saa 7 kasoro dakika 20.

Hii kwa kiingereza tunasema " It's twenty to one.

Yani tunataja dakika za kasoro alafu tunataja lisaa linalofuata.

 _Mifano zaidi_ :

* 2:35 - It's twenty-five to three.
( Ni saa tisa kasoro dakika 25 )

* 11:20 - It's twenty past eleven
( Ni saa tano na dakika ishirini )

* 4:18 - It's eighteen past four
( Ni saa kumi na dakika kumi na nane )

* 8:51 - It's nine to nine.
( Ni saa tatu kasoro dakika tisa )

* 2:59 - It's one to three.
( Ni saa tisa kasoro moja )

 QUARTER PAST / QUARTER TO ( NA ROBO / KASORO ROBO ) 

 QUARTER PAST - Na robo

* 7:15 - It's (a) quarter past seven.
( Ni saa  na robo )

 QUARTER TO - kasoro robo.

* 12:45 - It's a quarter to one.
( Ni saa saba kasoro robo )


 O'CLOCK - kamili

Tunatumia o'clock pale ambapo panapokuwa hakuna dakika (minutes )

* 10:00 - It's ten o'clock
( Saa 4 kamili )

* 5:00 - It's five o'clock.
( Ni saa 11 kamili )

* 1:00 - It's one o'clock.
( Ni saa 7 kamili )

Kuna muda tunaweza kuandika kama hivi - *NAMBA* + *O'CLOCK*

Mfano : 9 o'clock

SOMA PIA : Jifunze jinsi ya kutumia should, could na would

 12:00

Kwa 12:00 tunaweza tukasema kwa njia tatu.

1. Twelve o'clock
2. Midday - mchana
3. Midnight - usiku

 KUULIZIA MUDA .

Kwa kawaida huwa tunaulizia muda au saa kwa kutumia miundo hii :

* What time is it?
( Saa ngapi ? )

* What is the time ?
( Ni wakati gani? )
Njia ya adabu na heshima zaidi ya kuuliza saa kwa mtu mgeni usiemjua au mtu unayemuheshimu. 👇👇👇

* Could you tell me the time please?
( Tafadhali unaweza kuniambia wakati ? )

Could you tell me what time is it?
( Unaweza kuniambia ni saa ngapi sasa? )

Miundo ya kawaida ambayo tunatumia kuulizia wakati gani tukio fulani linatokea :

What time.........?
( Saa ngapi .......?

When......?
( Lini / wakati gani ........? )

* What time does the flight to New York leave?
( Ni saa ngapi ndege ya kwenda New York inaondoka? )

* When does the bus arrive from Mwanza?
( Wakati gani basi linawasiri kutoka Mwanza? )

* When does the concert begin?
( Wakati gani tamasha linaanza?)

 JINSI YA KUMUAMBIA MTU MUDA.

Tunatumia It is au It's kujibu swali la muda ( Right now )

* It is half past five ( 5:30 ).
- Ni saa 11 na nusu.

* It's ten to twelve ( 11:50 )
- Ni saa 6 kasoro dakika 10.

Tunatumia muundo wa  AT + TIME unapotaja muda wa tukio fulani.

* The bus arrives at midday (12:00).
- Basi linawasiri saa 6 mchana.

* The flight leaves at a quarter to two ( 1:45 ).
- Ndege inaondoka saa 8 kasoro robo.

* The concert begins at ten o'clock ( 10:00 )
- Tamasha linaanza saa 4 kamili

Pia tunaweza kutumia subject pronouns ( viwakilishi vya watenda ) kujibu maswali hayo:

* It arrives at midday ( 12:00 ).
- Linawasiri saa 6 mchana.

* It leaves at a quarter to two (1:45 ).
- Inaondoka saa 8 kasoro robo.

* It begins at a ten o'clock ( 10:00)
- Linaanza saa 4 kamili.


 AM vs. PM

Kikawaida huwa hatutumii masaa 24 katika kiingereza.

Tunatumia a.m kuanzia saa 6 usiku hadi saa 5 na dakika 59 asubuhi.

Tunatumia p.m kuanzia saa 6 mchana hadi saa 5 na dakika 59 usiku.


Tufuatilie :

Facebook : English Kona
Twitter : English Kona
Instagram : English Kona
YouTube : English Kona
WhatsApp : +255767 329 643
Read More

Wednesday, 22 May 2019

Jifunze jinsi ya kutumia SHOULD, COULD na WOULD

01:07 0

Karibu Englishkona.com kujifunza lugha ya kiingereza. Leo tumekutana tena kupeana mawili matatu katika lugha ya kiingereza.

Watu wengi wanaojifunza lugha ya kiingereza inakuwa ngumu kwao kuweza kutofautisha matumizi ya should, could na would. Siku ya leo tumekuwekea video inayoelezea jinsi ya kutumia should, could na would kwa ufasaha kabisa.

Video hii ni ya dakika 3 tu, imeelezea vizuri na kiundani kabisa jinsi ya kutumia maneno haya.

Pia English Kona inapenda kuwatangazia kuwa inatoa kozi ya kiingereza online kupitia  WhatsApp , kozi ni miezi minne na kila mwezi utalipia sh.10,000. Wasiliana nasi : +255767 329 643.

Tazama video  👇👇👇 :

Follow us :

Facebook : English Kona
Instagram : English Kona
Twitter : English Kona
YouTube : English Kona 
WhatsApp : +255 767 329 643

Read More

Saturday, 18 May 2019

VIDEO : Jinsi ya kutamka I'LL , YOU'LL, HE'LL, SHE'LL, IT'LL na THEY'LL.

02:45 0


Tafadhali SUBSCRIBE channel yetu.


Facebook : English Kona
Instagram : English Kona
YouTube : English Kona
WhatsApp : +255767329643

Read More

Wednesday, 8 May 2019

Jinsi ya kutamka WHERE , WERE na WE'RE.

20:22 0

Jifunze jinsi ya kutamka maneno haya kwa ufasaha kabisa.


Tafadhali subscribe channel yetu kwa kubofya hapa.

Read More

Monday, 29 April 2019

Welcome to English Kona

06:06 0


Tafadhali Subscribe channel yetu ya YouTube kupata mafunzo ya lugha ya kiingereza.
Read More

Post Top Ad