Header Ads Widget

Jifunze grammar : Noun

NOUN 


Unapoanza kujifunza kiingereza unatakiwa ujue baadhi ya kanuni muhimu ya lugha hii . Kanuni hizo utazijua baada ya kujifunza grammar .

Grammar itakusaidia kutunga sentensi zako kwa usahihi na pia itakufanya uweze kumudu kiingereza cha kuongea na kuandika .

Katika somo letu la leo utajifunza kitu cha kwanza kabisa katika grammar ambacho kinaitwa NOUN .

NOUN - ni neno ambalo linataja majina ya watu, vitu , mahali au wazo . Hivyo kwa kifupi " nouns " ni majina .

Kwa mfano :

Asha , Zena , Nasra , John , Anna , president , teacher , pilot , dog , cat , dog , cow , elephant , Dar es salaam, Tanzania , Italy , Uganda , hapiness , truth , danger .

1. KANUNI KATIKA MAJINA YA WATU NA MAHALI .

=>Katika uandishi majina ya watu huwa tunaanza kwa herufi kubwa , kama hivi : John , Abdul , Alex ...... Na sio john , abdul , alex .

=>Pia majina ya mahali huwa tunaanza kwa herufi kubwa , kama hivi : Tanzania , Uganda , Dodoma , Mwanza , Mtwara , Nairobi , South Africa ........ Na sio tanzania , uganda , dodoma , mwanza .

2. KANUNI KATIKA MAJINA MENGINE

=>Majina mengine kama ya wanyama , vitu n.k . Huwa tunaanza na herufi kubwa endapo tu ikiwa mwanzo wa sentensi tu , ila ikiwa katikati hatuanzi na herufi kubwa .

=>Kikawaida majina haya huanza na kiashairia ( article ) kwanza kama A , An na The .

MFANO :

A doctor , the car , an umbrella , a train , a book , the boss , a house , a bus ,..n.k
( Somo la mbele nitakufundisha jinsi ya kutumia hivyo viashiria au articles )

MIFANO YA NOUN KATIKA SENTENSI 

1. Juma likes reading books .
- Juma anapenda kusoma vitabu .

2. Asha wants to become a doctor
- Asha anataka kuwa daktari .

3. Yesterday I bought a new smartphone .
- Jana nilinunua simu janja mpya .

4. We have a cat in our home .
- Tuna paka nyumbani kwetu .

5. Asha lives in Tanzania .
- Asha anaishi Tanzania

Soma : Umoja na wingi wa majina ( singular and plural of nouns

Post a Comment

0 Comments