Present perfect tense - English Kona

Hot

Post Top Ad


Wednesday, 9 January 2019

Present perfect tenseThe present perfect tense ni moja wapo ya nyakati muhimu sana ambayo unatakiwa kuifahamu wakati unapoanza kujifunza lugha ya kiingereza .

Nyakati hii tunaitumia kuzungumzia mambo ambayo tayari yameshafanyika tayari ( au yameshakamilika kufanyika tayari au tukio ambalo limekamilika kufanyika ) .

MUUNDO WA SENTENSI ZA " THE PRESENT PERFECT TENSE " .

1. Sentensi za kukubali/ chanya

SUBJECT + HAS / HAVE +MAIN VERB

Ufafanuzi

" Has " inatumika kwa nafsi ya tatu umoja, yani => He , she na It .

" Have " inatumika kwa => I , You , We na They .

Main verb - hiki ni kitenzi kikuu , katika tense hii huwa tunatumia vitenzi ambavyo vipo katika muundo wa past participle . Mara nyingi huwa vinaishia na ED .

2. Sentensi za kukanusha/hasi

SUBJECT + HAS / HAVE + NOT + MAIN VERB .

Mfano : I have not done ( sijafanya ) .

3. kwa sentensi za kuuliza maswali

HAS / HAVE +  SUBJECT + MAIN VERB

Examples :

Have you finished ?
( umemaliza ?)

Have they done it ?
( wameifanya ? )

VIFUPISHO VINAVYOTUMIKAKATIKA PRESENT PERFECT TENSE .

I have = I've
You have = You've
He has = He's
She has = She's
It has = It's
We have = We've
They have = They've

SASA TUANGALIE BAADHI YA MIFANO YA SENTENSI ZA NYAKATI HII .

1. You've told me that before .
( Uliniambia hilo kabla .)

2. She has seen it .
( Ameiona )

3. You have eaten my food .
( Umekula chakula changu )

4. We have not played football .
( Hatujacheza mpira )

5. Have they done it ?
( Wameifanya ? )

6. He's seen Harry Potter .
( Ameiona Harry Potter )

Jinsi ya kutumia SINCE na FOR

Mara nyingi huwa tunatumia SINCE na FOR katika tense hii

đŸ‘‰ Tunatumia FOR kuongelea kipindi cha muda , mfano : For 6 years , for 2 hours , for 4 weeks , for 8 minutes ... N.k

đŸ‘‰Tunatumia SINCE kuongelea muda wa kitu kuanza ... SINCE ( tangu ) . Mfano : Since yesterday ( tangu jana ) , since wednesday ( tangu jumatano ) n.k

Mifano zaidi

I have been here since morning
( Nimekuwa hapa tangu asubuhi )

He has worked here since 2001.
( Amefanya kazi hapa tangu mwaka 2001 )

I have worked here for 3 years
( Nimefanya kazi hapa kwa miaka mitatu )

She has known your parents for long time .
( Amewajua wazazi wako kwa muda mrefu ) .
..……...............................................
Tembelea englishkona.com kila siku ili uweze kupata mafunzo ya kiingereza .

No comments:

Post a comment

Post Top Ad

UJUMBE MUHIMU KWA AJILI YAKO WEWE MSOMAJI:

"TUNAWASAIDIA WATU KUJIFUNZA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA KWA KUJIAMINI ZAIDI KUPITIA WHATSAPP"