Present perfect continuous tense - English Kona

Hot

Post Top Ad


Thursday, 10 January 2019

Present perfect continuous tenseTumeshasoma tayari " present perfect tense " . Sasa leo tuangalie " The present perfect continuous tense " .

Present perfect continuous tense - nyakati hii hutumika kuonyesha vitendo ambavyo vipo katika hali timilifu inayoendelea ( Yani
kitendo kilikuwa kimefanyika lakini katika hali ya kuendelea ) .

JINSI YA KUTENGENEZA SENTENSI ZA " PRESENT CONTINUOS TENSE " .

1. Kwa sentensi za kukubali / chanya

SUBJECT + HAS / HAVE + BEEN + MAIN VERB + ING

Ufafanuzi

MAIN VERB - Hiki ni kitenzi kikuu , kitenzi hiki tunaongeza ING mbele . Mfano : live / living , go / going , see / seing .

" Have " inatumika na I , You , We na They ( Nafsi ya kwanza umoja , na nafsi zingine isipokuwa nafsi ya tatu umoja )

" Has " inatumika na He , She na It.

Mfano :

I have been living here for 2 years
( Nimekuwa nikiishi hapa kwa miaka miwili ) .

She has been working here for 4 months .
( Amefanya kazi hapa kwa miezi minne )

2. Kwa sentensi za kukanusha / hasi
SUBJECT + HAS / HAVE + NOT + MAIN VERB + ING

Mfano : I have not been ......

3. Kwa sentensi za kuuliza maswali

HAS / HAVE + SUBJECT + MAIN VERB + ING

Mfano : Have you been.......

MIFANO ZAIDI .

I have been waiting for you 4 hours .
( Nimekuwa nikikusubiri kwa masaa
manne )

I'm tired because I have been running .
( Nimechoka kwa sababu nimekuwa
nikikimbia )

You have been talking to him since
morning .
( Umekuwa ukiongea nae tangu asubuhi )

It has not been raining.
( Haikuwa ikinyesha )

We have not been playing football .
( Hatukuwa tukicheza mpira )

You don't understand now because you
have not been listening
( huelewi sasa kwa sababu haukuwa
ukisikiliza .)

Have they been doing this work ?
( je , wamekuwa wakifanya kazi hii )

***************************
Usiache kutembelea Englishkona.com kila siku ili upate mafunzo ya kiingereza kila siku.....Pia jiunge na kozi yetu kwa kubofya hapa 👉👉EnglishKona Fluency Club

1 comment:

  1. w88 | fb88 | fb88 | hlv88 | w88.com | When his number came up, Kepa reacted by waving away Cabellero and insisting he was fine to continue , which sent Sarri into a fit of rage on the touchline. k8viet | casino888vn |    ReplyDelete

Post Top Ad

UJUMBE MUHIMU KWA AJILI YAKO WEWE MSOMAJI:

"TUNAWASAIDIA WATU KUJIFUNZA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA KWA KUJIAMINI ZAIDI KUPITIA WHATSAPP"