Tumeshasoma kuhusu simple present tense . Sasa hapa tunaangalie " the present continuous tense . "
Vitenzi vya " the present continuous tense " huwa vinaongezewa ING mbele.
MUUNDO WA SENTENSI ZA PRESENT CONTINUOUS TENSE :
Hapa tuna miundo mitatu ya sentensi ambayo ni :
1. Sentensi za kukubali / chanya
2. Sentensi za kukanusha
3. Sentensi za kuuliza maswali
1. Sentensi za kukubali / chanya
SUBJECT + AM / IS / ARE + MAIN VERB+ING
Ufafanuzi
AM - inatumika na I
IS - inatumika na nafsi ya tatu umoja , yani " He, she na It " .
ARE - inatumika na " You , We na They"
Examples :
I am cleaning my room
( Nina safisha chumba changu )
She is listening music now
( Anasikiliza mziki sasa )
They are waiting for me .
( Wananisubiria mimi )
You are watching TV
( Unaangalia TV )
2. Sentensi za kukanusha
SUBJECT + AM / IS / ARE + NOT + MAIN VERB + ING
Examples :
She is not eating food .
( hali chakula . )
He is not watching television .
( Haangalii runinga . )
I am not reading a book now
( Sisomi kitabu kwa sasa . )
3 . Sentensi za kuuliza maswali
Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :
AM / IS / ARE + SUBJECT + MAIN VERB + ING
Examples :
Is he watching TV ?
( je , anaangalia TV ? )
Are they waiting for john ?
( je wanamsubiria john ? )
MATUMIZI YA THE PRESENT CONTINUOUS TENSE ( WAKATI ULIOPO UNAOENDELEA ) :
1. Kwa vitendo au vitu ambavyo vinaendelea kwa sasa yani muda huu .
Examples :
They are eating right now .
( wanakula chakula sasa hivi . )
I am learning to drive a car .
( Ninajifunza kuendesha gari . )
He is living with his sister until he finds a room .
( Anaishi na dada yake mpaka pale atakapopata chumba . )
2.Tunatumia kuongelea vitu vijavyo au vitakavyofanyika wakati ujao.
Pia tunaweza kutumia the present continuous tense kuongela mambo yajayo - kama tukiongezea neno la wakati ujao kama vile : tomorrow , next year , next week n.k .
Tunatumia present continuous tense kuongelea vitu vijavyo ikiwa tayari tushaamua na tushapanga kabla ya kuongea .
Examples :
I am starting my new job next month
( ninaanza kazi yangu mpya mwezi ujao )
We are eating at mama ntilie tonight . We have already booked the table .
( Tunakula kwa mama ntilie usiku . Tayari tushaweka ( oda ) .... )
When you are starting your new job ?
( Lini unaanza kazi yako mpya ? )
SHERIA ZA VITENZI KATIKA PRESENT CONTINUOUS TENSE .
Vitenzi vya present continuous tense huwa tunaongezea " ING " katika kitenzi kikuu ( main verb )
Mfano : go / going , do / doing , look / looking , read / reading , stay / staying .
- Ila kwa vitenzi ambavyo vinaishia E , huwa tunaondoa E na kuongezea ING , Mfano : come / coming , mistake / mistaking .
- Kwa vitenzi ambavyo vinaishia na IE , huwa tunabadilisha IE kuwa Y . Mfano : lie / lying , die / dying .
****"*"*"*"*”"**""""""
Bofya hapa kujiunga na EnglishKona Fluency Club
No comments:
Post a Comment