PRONOUNS ( VIWAKILISHI )
Haya ni maneno ambayo yanatumika kuwakilisha majina ( nouns ) .
Mifano ya pronouns ni kama vile :
I , You , She , He , It , We , They , Me , Yours , Ours , It's , Myself ,... N.K
Kwa leo tutasoma kwa uchache kwanza.
JINSI YA KUTUMIA PRONOUNS ( VIWAKILISHI )
Tunatumia maneno haya kuwakilisha majina ( Nouns ) . Kwa mfano badala ya kusema :
" Asha lives here "...... Tunaweza kusema ... " She lives here "
Angalia mifano hii :
Asha lives here = > She lives here
Anna and I are living here = > We are living here .
SASA HEBU TUANGALIE JINSI YA KUTUMIA PRONOUNS .
I - hii hutumika na nafsi ya kwanza umoja... Yani MIMI . Mfano : I live here ( Ninaishi hapa )
#Wingi wa nafsi hii ni " We " .
You ( wewe / ninyi ) - hii inatumika na nafsi ya pili umoja na wingi. Mfano : You are reading this story ( Unasoma hadithi hii / mnasoma hadithi hii )
#wingi wa nafsi hii ni " You " .
He ( yeye ) - hii hutumika kuwakilisha majina ya kiume ya nafsi ya tatu umoja . Mfano :
Juma is playing football = He is playing football
#Wingi wa kiwakilishi hiki ni " They " .
She ( yeye ) - Hii hutumika kuwakilisha majina ya kike ya nafsi ya tatu .
Mfano
Asha , Mwantumu , Mary , Anna , Irene , Vanessa , Mariamu ..... Majina haya huwakilishwa na " SHE " . Kwa mfano : Asha ( She ) likes football .
#Wingi wa nafsi hii ni " They " .
It - hii hutumika na nafsi ya tatu umoja lakini kwa majina ya vitu, wanyama na mimea .
For example :
Goat eats grass = It eats grass
# Wingi wa nafsi hii ni " They " .
MIfano zaidi ya pronouns ( viwakilishi )
I play football
They need us
We are together
I am listening to music
She loves her mother .
It started to rain .
Personal pronouns
Personal pronouns - Hivi ni viwakilishi vinavyotumika kuwakilisha majina maalumu ya watu au vitu .
For example : I , me , mine , you, yours , his , her , hers , we , they , or them .
Pronouns hizi zinagawanyika katika sehemu kuu nne kama zifuatazo :
Subjective pronouns
Objective pronouns
Possissive pronouns
Reflexive pronouns
Subjective pronouns
Hivi ni viwakilishi vya mtenda au watenda wa kitenzi ( verb ) , viwakilishi hivi ni kama vile , I , you , we , he , she , it na they .
I live here
He loves Mary
They saw Omary
Objective pronouns
Hivi ni viwakilishi vya mtendwa wa kitenzi .
He loves her
They saw him
She need us
Possessive pronouns .
Hivi ni viwakilishi ambavyo vinatumika kuonyesha umiliki wa vitu kwa watu .
That bag is mine
( Begi lile ni la kwangu )
Take your money
( chukua pesa yako )
She will give her book
( Atampa kitabu chake )
Reflexive Pronouns
Viwakilishi hivi ni kama vile , myself , himself , herself , itself , ourselves, yourselves , and themselves .
Myself ( mi mwenyewe )
Himself ( ye mwenyewe )
Herself ( ye mwenyewe )
Itself( chenyewe / ye mwenyewe )
Yourselves ( we mwenyewe )
Themselves ( wao wenyewe )
Juma prepared himself for the journey
They will know themselves
She fell and hurt herself .
No comments:
Post a Comment