Header Ads Widget

Verbs ( vitenzi )Verb ni neno linalotaja kitendo , kwa mfano :-

to do-  kufanya  ,
run - kimbia  ,
sleep - lala ,
walk - tembea  ,
 hit - gonga ....n.k

Verb inapokuwa kwenye hali yake halisi huitwa " infinitive " . Mara nyingi huwa inakaa mbele ya neno  to .

For example :

She began to run ( alianza kukimbia )

I decided to follow you ( niliamua kukufuata )

MIFANO ZAIDI YA VITENZI

1. I speak english well ( naongea kiingereza vizuri )

2. I am watching television ( naangalia tv )

3.  I will call you later ( nitakupigia baadae )

4. I will help you ( nitakusaidia )

5. I bought a new smartphone yesterday ( Jana nilinunua smartphone mpya )

6. She walks very slowly ( huwa anatembea taratibu sana )

7. I ate food ( nilikula chakula )

8. I jumped into the river ( nilirukia mtoni )

9. She is reading a book . ( anasoma kitabu )

10. He will beat you ( atakupiga )

11. Goat eats grass ( Mbuzi hula majani)

AUXILIARY VERBS( Vitenzi visaidizi )

Hivi ni vitenzi ambavyo vinasaidia kuunda tenses, moods na voices vya vitenzi vingine . vitenzi hivyo ni be, do na have .

BE ( am , is , are , was , were , been , being ) - hutumika na vitenzi vingine kuunda continuous tenses (nyakati zinazo endelea) na passive voices .

She was living here .
( Alikuwa anaishi hapa )

They were eating food .
( Walikuwa wanakula chakula )

Kenya were beaten by Tanzania in the final .

HAVE - hutumika kutengeneza perfect tenses ( nyakati timilifu )

I have been living with him for 2 years .
( Nimekuwa nikiishi nae kwa miaka miwili )

She has done .

DO hutumika :

kuweka msisitizo katika sentensi .

They did look tired .

- Kuuliza maswali

Do you work here ?

- kutengeneza sentensi za kukanusha .

I don't like meat .

TUTAFAHAMU ZAIDI KUHUSU " VERB " TUTAPOANZA KUJIFUNZA " TENSES " .

👉👉Englishkona.com

Post a Comment

0 Comments