COUNT NOUNS
- Ni majina yote ambayo yanaweza kuhesabika .
# Mfano:
Pen , computer , bottle , spoon, cup , television , chair , shoe , finger , camera , table , book...
SIFA YA MAJINA HAYA ( COUNT NOUNS )
I > Majina haya yana wingi :
#Mfano
Pens , computers , bottles , spoons , cups , televisions , chairs , shoes , fingers , cameras , books , tables ....
II > Yanaweza kuelezwa kwa kutumia :
a few , few , many , some , every , each , these , the number of .
Mfano :
a few pens , a few computers , many bottle , some spoons , each cup , these television , the number of chairs , a few shoes , a few fingers , some cameras , these books , the number of tables ....
III > Yanatumia viashiria ( articles ) :
A , AN na THE .
# Kumbuka
Huwa tunatumia viashiria ikiwa jina lipo kwenye umoja .
#Mfano :
a pen , the computer, a bottle , the spoon , the cup , a television , the chair , a shoe , the finger , the camera , a book , the table ......
IV > Majina haya hayatumii MUCH ( kwa mfano huwezi kusema " much chairs au much computers ) .
MAJINA YASIYOHESABIKA ( NON-COUNT NOUNS )
- Haya ndiyo majina yasiyohesabika . Kikawaida majina haya huelezwa kwenye makundi au aina .
#Mfano :
water , wood , ice , air oxygen , English , Swahili , traffic , furniture , milk , wine , sugar , rice , meat , flour , soccer , sunshine ,...n.k
SIFA ZA MAJINA HAYA :
I > Kikawaida hayawezi kuwekwa kwenye wingi .
II . Yanaweza yakatumia viashiria ( A , AN au THE ) au yasitumie viashiria , hapa inategemea na sentensi yenyewe .
For example :
- Sugar is sweet .
( sukari ni tamu )
- The sunshine is beutiful .
( Mwanga wa jua ni mzuri )
- I drink milk .
( Huwa nakunywa maziwa )
- He eats rice .
( Huwa anakula wali )
- We watch soccer together .
( Huwa tunaangalia mpira pamoja )
- The wood is burning .
IV . Yanaweza kuelezwa kwa kutumia :
SOME , ANY , ENOUGH , THIS , THAT na MUCH .
For example :
- We ate some rice and milk
( Tulikula wali na maziwa )
- I hope to see some sunshine today
( Leo natumaini kuona mwanga wa jua )
- This meat is good .
( Nyama hii ni nzuri )
- She does not speak much swahili
( Haongei kiswahili sana )
- Do you see any traffic on the road ?
( Je unaona foleni yoyote barabarani ? )
- That wine is very old .
( Wine hiyo ni ya zamani sana )
0 Comments