MAJINA YA UMILIKI ( POSSESSIVE NOUNS )
Possessive nouns - haya ni majina yanayotumika kuonyesha umiliki wa vitu .
=>Kikawaida majina haya huongezewa alama ya mkato wa juu ( ' ) na S .
#Mfano :
- Anna's car
( Gari la Anna )
- Juma's wife
( Mke wa Juma )
- Zena's house
( Nyumba ya Zena )
- Mother's mirror
( Kioo cha mama )
=> Kwa majina ya wingi ambayo yanaishia na S , huwa tunaweka mkato wa juu baada ya hiyo S .
#Mfano :
- My parents' house
( Nyumba ya wazazi wangu )
- The kids' toys
=> Kama watu wawili wana miliki kitu kimoja , basi ongeza alama ya mkato wa juu ( ' ) na S kwa jina la mtu wa pili .
#Mfano:
- John and Mary's new house
( Nyumba mpya ya John na Mary )
- Asha and Anna's car
( Gari la Asha na Anna )
=>Kama watu wawili wana miliki vitu viwili tofauti , basi kila mmoja utamuongezea alama ya mkato wa juu ( ' ) na S .
#Mfano
-John's and Dan's pants
( kaptura za John na Dan )
- Ben's and Jim's offices
( Ofisi za Ben na Jim )
*****************************
No comments:
Post a Comment