Simple Past Tense - English Kona

Hot

Post Top Ad


Friday, 1 February 2019

Simple Past TenseSIMPLE PAST TENSE ( WAKATI ULIOPITA ) .

Tunatumia "Simple past tense" kuongelea vitu , vitendo au hali iliyotokea wakati uliopita. Vitendo hivyo vinaweza kuwa vya muda mrefu au mfupi.

 MIFANO YA VITENDO VYA MUDA MFUPI .

She went to the hospital
( Alienda hospitalini )

We did not hear telephone.
(Hatukusikia simu.)

The car exploded at 9:30 AM.
(Gari liliripuka saa 3: 30 asubuhi.)

 MIFANO YA VITENDO VYA MUDA MREFU .

I lived in South Africa for 10 years.
(Nimeishi South Africa kwa miaka 10.)

We did not sing at the concert.
(Hatukuimba katika tamasha.)

 MIUNDO YA SENTENSI ZA "SIMPLE PAST TENSE"

Tuna miundo mitatu ya sentensi za "SIMPLE PAST TENSE" nayo ni :

1. Sentensi za kukubali / chanya.
2. Sentensi za kukanusha .
3. Sentensi za kuuliza maswali .


1. SENTENSI ZA KUKUBALI

Muundo wa sentensi za kukubali unakuwa hivi :

Mtenda + verb

Ufafanuzi :

Mtenda  = > I , You , She , It , We na They , Asha , John , Mariamu ,....

MAIN VERB ( kitenzi kikuu ) = > Kitenzi hiki kinakuwa katika hali ya " Simple Past " hivyo mara nyingi huwa vinaishia na " ED " .

Mifano ya sentensi :

You worked very hard .
( Ulifanya kazi kwa bidii . )

I went to London.
(Nilienda London.)

She was here.
(Alikuwa hapa .)

I lived here when I was young.
(Niliishi hapa pindi nilivyokuwa mdogo.)

2. SENTENSI ZA KUKANUSHA

Muundo wa sentensi za kukanusha unakuwa kama hivi .

Mtenda + did + not +  verb(infinitive)

Ufafanuzi :

kitenzi ambacho kitatumika kitakuwa kati hali yake halisi (Infinitive) - Yani hakibadiliki ... Kwa mfano , go / go , see / see , watch / watch .............Yani havibadiliki .

Mifano ya sentensi :

She did not go with me.
(Hakuenda na mimi.)

I did not hate them.
(Sikuwachukia.)

They did not see that car.
(Hawakuliona gari hilo.)

Mary did not go to work yesterday.
(Mary hakuenda kazini jana.)

3. SENTENSI ZA KUULIZA MASWALI 

Muundo wa kuuliza maswali unakuwa kama hivi :

Did + mtenda + verb(infinitive)

Mifano ya sentensi

Did you want him to teach you?
(Ulimtaka akufundishe?)

Did they live here?
(Je waliishi hapa?)

Did you go with him?
(Ulienda naye?)

Did she see that accident?
(Je aliiona ajali hiyo?)

Did he watch TV last night?
(Je aliangalia TV usiku uliopita?)

 JINSI YA KUTUMIA " SIMPLE PAST "KWA KUTUMIA MAIN VERB BE (KUWA)

VERB BE - zinazotumika katika Simple Past ni "was" na "were"

Was - inatumika kwa nafsi ya kwanza na tatu umoja , yani I , He , She , It .

Were - inatumika kote isipokuwa tu nafsi ya tatu umoja .... Hivyo " Were " inatumika kwa You , We na They .

Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :

SUBJECT + WAS / WERE + MAIN VERB + ING

Ufafanuzi :

Kama ukitumia kitenzi "be" pamoja Main verb ... Basi Main verb lazima uongezee " ING " mbele . Kwa mfano : was going , were going n.k .

Mifano ya sentensi :

You were in Tanzania.
(Ulikuwa Tanzania.)

She was not happy yesterday.
(Hakuwa na furaha jana.)

They were late.
( Walikuwa wamechelewa .)

Was I right?
(Je nilikuwa sahihi?)

I was loving her.
(Nilikuwa nampenda.)

Were you angry?
( Ulikuwa na hasira?)

No comments:

Post a comment

Post Top Ad

UJUMBE MUHIMU KWA AJILI YAKO WEWE MSOMAJI:

"TUNAWASAIDIA WATU KUJIFUNZA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA KWA KUJIAMINI ZAIDI KUPITIA WHATSAPP"