Header Ads Widget

Makosa katika kiingereza : Double negativesDouble negatives -  haya ni maneno mawili hasi ( ya kukanusha ) ambayo yanatumika katika sentensi moja . Kwa kutumia double negatives kunapelekea sentensi kubadilika kuwa sentensi chanya ( ya kukubali ) .

Katika kiingereza huwa hatutumii double negatives kwa sababu sentensi zinakuwa zinachanganya na pia zinakuwa zipo katika grammar ( sarufi ) ambayo si sahihi .

MFANO :

USISEME : " i didn't buy nothing at the store "
( sijanunua chochote dukani )

SEMA : " I didn't buy anything at the store "
( Sijanunua chochote dukani )
Kama hapo juu nilivyoelezea kuwa katika kiingereza huwa hatuna double negatives " ( not + no ) katika sentensi , badala yake huwa tunatumia " any- " .

➡ I don't know anyone at this party .
 I don't know no one at this party .
( Simjui yoyote katika sherehe hii )

➡We are not doing anything at the moment .
We are not doing nothing at the moment .
( Hatufanyi chochote kwa sasa )

➡Don't worry, he won't tell anybody your secret .
Don't worry , he won't tell nobody your secret .
( Usijali , hatamuambia mtu yoyote siri yako )

➡ I can't go anywhere tonight .
I can't go nowhere tonight .
( Siwezi kwenda popote usiku )

➡  We saw nothing .
We didn't see nothing .
( Hatukuona chochote )


" FUTA MAKOSA YAKO YOTE AMBAYO UNAYAFANYA KATIKA LUGHA YA KIINGEREZA NA UWEZE KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA KUJIAMINI KABISA......KUJUA ZAIDI BOFYA HAPA "Post a Comment

1 Comments