Year Old au Years Old ? - English Kona

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, 1 March 2019

Year Old au Years Old ?Makosa ambayo unaweza ukawa unayafanya wakati wa kuzungumza kuhusu umri ( age )

 Usiseme : My son has six years

 Usiseme : My son has six years old

 Sema : My son is six years old .

 Pindi tunapokuwa tunaongelea kuhusu umri ( age ) huwa tunatumia  ( am , is , are , was na were ) ... Hatutumii Has au Have .

Mfano :

I'm twenty years old
( Nina miaka thelathini )

My daughter is fourteen years old
( Binti yangu ana miaka 14  )

These houses are 80 years old .
( Nyumba hizi zina miaka 80 )

I was five years old
( Nilikuwa nina miaka tano )

You were eight years old
( Ulikuwa una miaka nane )

 Pia tunaweza kutumia am / is / are + age .... Bila ya kutumia years old

My nephew is fourteen
( Mpwa wangu ana miaka 14 )

I'm thirty ( Nina miaka 30 )

My kids are  five and six
( Watoto wangu  wana miaka tano na sita )

 Kama ikiwa siku ya mtu kuzaliwa , tunatumia turn_age  ( Yani anatimiza umri... )

Mfano :

My cousin just turned three
( Binamu ametimiza miaka mitatu )

My wife is turning twenty seven next week .
( Mke wangu anatimiza miaka ishirini na saba ( 27 ) wiki ijayo )

 Ikiwa umri wa mtu umetumika kama adjective yani kabla ya jina lake , basi hapa tunatumia year old na sio years old .

 My seven years old daughter is starting school next week

My seven year old daughter is starting school next week .
( Binti wangu wa miaka saba anaanza shule wiki ijayo )

****************************

Futa makosa yote ambayo unayafanya katika lugha ya kiingereza , ongea sasa kiingereza kwa ufasaha bila ya kufanya makosa .... Jiunge sasa katika kozi yetu kwa gharama ya shilingi 10000 tu  kwa mwezi ....Wasiliana nasi 0767329643

 Karibu sana

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad