Header Ads Widget

Jinsi ya kusoma saa kwa kiingereza. ( Time telling )Karibu tena English Kona kujifunza mawili matatu katika lugha ya kiingereza. Katika somo letu la leo tutajifunza jinsi ya kusoma na kutaja muda katika lugha ya kiingereza.

Kabla hatujaendelea , tujikumbushe hili usomaji wa saa za kiingereza ni tofaut na kiswahili ... Kwa mfano ikiwa 7 kwa kiswahili tunasema moja.

 _Angalia vizuri hapa_ :

1 = 7
2 = 8
3 = 9
4 = 10
5 = 11
6 = 12
7 = 1
8 =  2
9  =  3
10 = 4
11 = 5
12 = 6

Lakini katika kiingereza huwa tunataja namba kama zilivyo.

 JINSI YA KUTAJA NA KUSOMA MUDA.

Kuna njia mbili za kutaja mda

1. Kuanza kutaja saa kwanza alaf dakika. ( Hour + Minutes )

* 6:25 - It's six twenty-five.
- Ni saa kumi na mbili na dakika ishirini na tano.

* 9:05 - It's nine O-five ( O inatamkwa kama herufi O )
- Ni saa tatu na dakika  tano.

* 9:11 - It's nine eleven.
- Ni saa tatu na dakika kumi na moja.

2. Kutaja dakika kwanza alafu saa.
( Minutes + PAST / TO + Hour )

Kwa dakika 1-30 tunatumia PAST baada ya kutaja dakika.

Kwa dakika 31-59 tunatumia  TO baada ya kutaja dakika.

 _FAHAMU HILI_ :

Tunapotumia TO ina maana tunazungumzia kasoro. Sasa kwa mfano :

12 : 40 - saa 7 kasoro dakika 20.

Hii kwa kiingereza tunasema " It's twenty to one.

Yani tunataja dakika za kasoro alafu tunataja lisaa linalofuata.

 _Mifano zaidi_ :

* 2:35 - It's twenty-five to three.
( Ni saa tisa kasoro dakika 25 )

* 11:20 - It's twenty past eleven
( Ni saa tano na dakika ishirini )

* 4:18 - It's eighteen past four
( Ni saa kumi na dakika kumi na nane )

* 8:51 - It's nine to nine.
( Ni saa tatu kasoro dakika tisa )

* 2:59 - It's one to three.
( Ni saa tisa kasoro moja )

 QUARTER PAST / QUARTER TO ( NA ROBO / KASORO ROBO ) 

 QUARTER PAST - Na robo

* 7:15 - It's (a) quarter past seven.
( Ni saa  na robo )

 QUARTER TO - kasoro robo.

* 12:45 - It's a quarter to one.
( Ni saa saba kasoro robo )


 O'CLOCK - kamili

Tunatumia o'clock pale ambapo panapokuwa hakuna dakika (minutes )

* 10:00 - It's ten o'clock
( Saa 4 kamili )

* 5:00 - It's five o'clock.
( Ni saa 11 kamili )

* 1:00 - It's one o'clock.
( Ni saa 7 kamili )

Kuna muda tunaweza kuandika kama hivi - *NAMBA* + *O'CLOCK*

Mfano : 9 o'clock

SOMA PIA : Jifunze jinsi ya kutumia should, could na would

 12:00

Kwa 12:00 tunaweza tukasema kwa njia tatu.

1. Twelve o'clock
2. Midday - mchana
3. Midnight - usiku

 KUULIZIA MUDA .

Kwa kawaida huwa tunaulizia muda au saa kwa kutumia miundo hii :

* What time is it?
( Saa ngapi ? )

* What is the time ?
( Ni wakati gani? )
Njia ya adabu na heshima zaidi ya kuuliza saa kwa mtu mgeni usiemjua au mtu unayemuheshimu. 👇👇👇

* Could you tell me the time please?
( Tafadhali unaweza kuniambia wakati ? )

Could you tell me what time is it?
( Unaweza kuniambia ni saa ngapi sasa? )

Miundo ya kawaida ambayo tunatumia kuulizia wakati gani tukio fulani linatokea :

What time.........?
( Saa ngapi .......?

When......?
( Lini / wakati gani ........? )

* What time does the flight to New York leave?
( Ni saa ngapi ndege ya kwenda New York inaondoka? )

* When does the bus arrive from Mwanza?
( Wakati gani basi linawasiri kutoka Mwanza? )

* When does the concert begin?
( Wakati gani tamasha linaanza?)

 JINSI YA KUMUAMBIA MTU MUDA.

Tunatumia It is au It's kujibu swali la muda ( Right now )

* It is half past five ( 5:30 ).
- Ni saa 11 na nusu.

* It's ten to twelve ( 11:50 )
- Ni saa 6 kasoro dakika 10.

Tunatumia muundo wa  AT + TIME unapotaja muda wa tukio fulani.

* The bus arrives at midday (12:00).
- Basi linawasiri saa 6 mchana.

* The flight leaves at a quarter to two ( 1:45 ).
- Ndege inaondoka saa 8 kasoro robo.

* The concert begins at ten o'clock ( 10:00 )
- Tamasha linaanza saa 4 kamili

Pia tunaweza kutumia subject pronouns ( viwakilishi vya watenda ) kujibu maswali hayo:

* It arrives at midday ( 12:00 ).
- Linawasiri saa 6 mchana.

* It leaves at a quarter to two (1:45 ).
- Inaondoka saa 8 kasoro robo.

* It begins at a ten o'clock ( 10:00)
- Linaanza saa 4 kamili.


 AM vs. PM

Kikawaida huwa hatutumii masaa 24 katika kiingereza.

Tunatumia a.m kuanzia saa 6 usiku hadi saa 5 na dakika 59 asubuhi.

Tunatumia p.m kuanzia saa 6 mchana hadi saa 5 na dakika 59 usiku.

English Kona tunawasaidia watu wanaopenda kuongea kiingereza kwa ufasaha. Tunatoa mafunzo ya kiingereza online kwa njia ya WhatsApp, mafunzo hayo utayapata moja kwa moja kwenye simu yako na utasoma wewe na mwalimu kwa muda wako ambao unakuwa free.

Mafunzo yetu ni ya miezi minne na kila mwezi utakuwa unalipia sh.12,000 tu. Na mafunzo yetu ni mazuri sana kwani yatakusadia uweze kuongea kiingereza kwa ufasaha na kwa kujiamini kabisa. 

Na uzuri wa mafunzo yetu unajifunza mahala popote pale ulipo na kwa muda wako wowote ule uutakao ambao utakuwa free.

Jiunge leo kwa kuwasiliana nasi WhatsApp  : 0767 329 643Post a Comment

0 Comments