Header Ads Widget

"My" au "Mine" ? - Jifunze kutofautisha.
Katika grammar ya kiingereza tuna possessive adjectives na possessives nouns.

Possessive adjectives - Vivumishi vya umiliki.
( My , your , his , her , its , our  , their )

Possessive pronouns - Viwakilishi vya umiliki.
( Mine, yours , his , hers , its, ours , theirs )

Tunatumia maneno haya kuelezea au kutaja vitu ambavyo tunavimiliki. Sasa leo tujifunze ni wakati gani wa kutumia maneno haya kwa ufasaha. Baada ya kusoma somo hili basi utaweza kuyatumia maneno haya kwa usahihi.

Tumia  "MY" kabla ya jina au majina ya vitu tunavyomiliki na tumia  "MINE" baada ya jina au majina ya vitu tunavyomiliki.


* Anna is my friend.
(Anna ni rafiki yangu.)

* Anna is a friend of mine.
(Anna ni rafiki yangu.)

* Those are  my glasses.
( Hayo ni miwani yangu.)

* Those glasses are mine.
(Mawani hayo ni yangu.)

* This is my dog.
( Huyu ni mbwa wangu.)

* This dog is mine.
( Mbwa huyu ni wangu.)

* Your dog is bad. Mine is good.
( Mtoto wako ni mbaya. Wangu ni mzuri )

* This cat is mine not yours.
(Huyu paka ni wangu na sio wako.)


TUANGALIE MIFANO YA JUMLA YA POSSESSIVE ADJECTIVES NA POSSESSIVE PRONOUNS 👇👇👇

 MIFANO ZAIDI

1. This is his car. This car is his.
- Hili ni gari lake. Gari hili ni lake.

2. This is her ring. This ring is hers.
 - Hii ni pete yake. Pete hii ni yake.
( SIO : This ring is her. )

3. This is their radio. This radio is theirs.
- Hii ni radio yao. Redio hii ni yao.
( SIO : This radio is their. )

Jifunze pia jinsi ya kutofautisha kati ya "I" na "Me" 👇👇👇

Tazama hapa chini 👇👇👇


Unataka kuongea kiingereza kwa ufasaha ? Bofya hapa kujua zaidi => ENGLISH COURSE
Tufuatile :

Facebook, twitter na Instagram kwa jina la English Kona.

Post a Comment

0 Comments