Future Continuous Tense
(Wakati ujao hali ya kuendelea.)
The Future Continuous Tense ni nyakati ambayo
tunaitumia kuongelea vitendo ambavyo vitafanyika wakati ujao katika hali ya
kuendelea.
MIUNDO YA SENTENSI :
Kuna miundo hii ambayo ni :
1. Sentensi za kukubali / chanya
2. Sentensi za kukanusha
3. Sentensi za kuuliza maswali
1. Sentensi chanya
Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :
Mtenda + will + be + verb + ing
Examples :
I will
be working.
(Nitakuwa
nafanya kazi.)
You will be waiting here.
(Utakuwa
unasubiria hapa.)
Mary will be using the car.
(Mary atakuwa
anatumia gari.)
They will be cooking for us.
(Watakuwa
wanatupikia.)
Take your umbrella. It will
be raining when you return.
(Chukua
mwamvuli wako. Mvua itakuwa inanyesha ukirudi.)
2. Sentensi za kukanusha
Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi:
Mtenda + will + not + be + verb + ing
Examples :
I will
not be working here.
(Nitakuwa
sifanyi kazi hapa.)
Mary will not be using the car.
(Mary
atakuwa hatumii gari.)
You will not be waiting here.
(Utakuwa
hausubiri hapa.)
They will not be cooking for us.
(Watakuwa
hawatupikii.)
She will not be reading books.
(Atakuwa
hasomi vitabu.)
3. Sentensi za kuuliza maswali
Muundo wa sentensi hizi unakuwa hivi :
Will + Mtenda + be + verb + ing
Examples :
Will you be
playing football?
(Je!
utakuwa unacheza mpira?)
Will they be cooking for us?
(Je!
Watakuwa wanatupikia?)
Will Mary be using the car?
(Je! Mary
atakuwa anatumia gari?)
Will we be watching TV?
(Je!
Tutakuwa tunaangalia TV?)
0 Comments