The Future Perfect Continuous Tense hii ni nyakati ambayo inaelezea vitendo ambavyo vitafanyika wakati ujao. Tense hii hutumika kuonyesha vitendo ambavyo vipo katika hali timilifu inayoendelea (Yani kitendo kitakuwa kinafanyika katika hali timilifu lakini katika hali ya kuendelea.)
MIUNDO YA SENTENSI :
Kuna miundo mitatu (3) ambayo ni :
1. Sentensi za
kukubali / chanya
2. Sentensi za
kukanusha
3. Sentensi za kuuliza maswali
1. Sentensi chanya
Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :
Mtenda + will + have + been + verb + ing
Examples :
They will have been
living in Paris for five years.
(Watakuwa wamekuwa
wakiishi Paris kwa miaka mitano.)
Nasra will have been
reading this book since morning.
(Nasra atakuwa amekuwa
akisoma kitabu hiki tangu asubuhi.)
The doctor will have
been treating patients for two years.
(Daktari atakuwa
amekuwa akitibu wagonjwa kwa miaka miwili.)
He will have been
waiting here for three hours.
(Atakuwa amekuwa
akisubiri hapa kwa masaa matatu.)
Next year I will have
been working here for four years.
(Mwaka ujao nitakuwa
nimekuwa nikifanya kazi hapa kwa miaka minne.)
2. Sentensi za kukanusha
Muundo wa sentensi
hizi huwa hivi:
Mtenda + will + not +
have + been + verb + ing
MIFANO :
Mtenda + will + not + have + been + verb + ing
He will not have been
working in the factory for six months.
(Hatakuwa amekuwa
akifanya kazi katika kiwanda hiki kwa miezi sita.)
I will not have been
using the car .
(Sitakuwa nimekuwa
nikitumia gari.)
She will not have been
living here for three years.
(Hatakuwa amekuwa
akiishi hapa kwa miaka mitatu.)
My sister will not
have been listening to music for nine hours.
(Dada yangu hatakuwa
amekuwa akisikiliza muziki kwa masaa tisa.)
He won't have been
using his camera for two days.
(Hatakuwa amekuwa
akitumia kamera yake kwa siku mbili.)
3. Sentensi za kuuliza maswali
Will he have been
loving her for five years?
(Je! Atakuwa amekuwa
akimpenda kwa miaka mitano?)
Will she have been
studying in the new college since December?
(Je! Atakuwa amekuwa
akisoma katika chuo kipya tangu December?)
Will they have been
working in this factory since June?
(Je! Watakuwa
wamefanya kazi katika kiwanda hiki tangu Juni?)
Will you have been
eating vegetables for three months?
(Je! Utakuwa umekuwa
ukila mboga za majani kwa miezi mitatu?)
0 Comments