Future Perfect Tense - English Kona

Hot

Post Top Ad


Wednesday, 23 September 2020

Future Perfect TenseThe Future Perfect Tense ni nyakati ambayo tunaitumia kuongelea vitendo ambavyo vitafanyika wakati ujao katika hali ya timilifu.

MIUNDO YA SENTENSI :


Kuna miundo  hii ambayo ni :

1. Sentensi za kukubali / chanya
2. Sentensi za kukanusha
3. Sentensi za kuuliza maswali


1. Sentensi chanya

Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :

Mtenda +  will + have + verbExamples :


I will have finished.

(Nitakuwa nimemaliza.)

She will have started a new job.

(Atakuwa ameanza kazi mpya.)

They will have bought a new laptop.

(Watakuwa wamenunua laptop mpya.)

Mary will have written a letter.

(Mary atakuwa ameandika barua.)

I will have arrived.

(Nitakuwa nimefika.)

2. Sentensi za kukanusha


Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi:


Mtenda + will + not + have + verb


Examples :


She will not have gone to work.

(Atakuwa hajaenda kazini.)

We will not have left.

(Hatutakuwa tumeondoka.)

They will not have received it.

(Hawatakuwa wameipokea.)

He will not have gone to school.

(Hatakuwa ameenda shule.) 

You will have not worked.

(Hautakakuwa umefanya kazi.)


3. Sentensi za kuuliza maswali


Muundo wa sentensi hizi unakuwa hivi :


Will + Mtenda + be + verb + ing


Examples :


Will you have arrived?

(Je utakuwa umefika?)

Will they have worked?

(Je watakuwa wamefanya kazi?)

Will you have finished?

(Je utakuwa umemaliza?)

Will Anna have gone to work?

(Je Anna atakuwa ameenda kazini?)

MIFANO ZAIDI  :


I'll have finished when you arrive.

(Nitakuwa nimemaliza ukifika.)

She'll have forgotten everything.

(Atakuwa amesahau kila kitu.)

We will not have worked.

(Hatutakuwa tumefanya kazi.)

No comments:

Post a comment

Post Top Ad

UJUMBE MUHIMU KWA AJILI YAKO WEWE MSOMAJI:

"TUNAWASAIDIA WATU KUJIFUNZA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA KWA KUJIAMINI ZAIDI KUPITIA WHATSAPP"