Past Continuous Tense - English Kona

Hot

Post Top Ad


Monday, 14 September 2020

Past Continuous Tense

Tense hii tunatumia kuongelea vitendo ambavyo vimefanyika wakati uliopita ambavyo vilikuwa katika hali ya kuendelea.

Mfano: I was eating. (Nilikuwa nakula.)

Verbs vyetu katika tense hii huwa tunaongezea ING mbele.

Sasa tuangalie jinsi ya kutengeneza au kuunda sentensi katika nyakati hii.

MIUNDO YA SENTENSI  

Kama kawaida huwa tuna miundo mitatu ya sentensi ambayo ni :

1. Sentensi za kukubali / chanya
2. Sentensi za kukanusha
3. Sentensi za kuuliza maswali

1. Sentensi chanya

Mtenda + was / were + verb + ing

Ufafanuzi

Jinsi ya kutumia WAS na WERE

WAS - inatumika na I, he, she, it na jina la umoja.
WERE - inatumika na you, we, they na majina ya wingi.

Jinsi inavyokuwa :

I was - Nilikuwa
she was - alikuwa
he was - alikuwa
it was - alikuwa / kilikuwa / ilikuwa
John was - John alikuwa
Asha was - Asha alikuwa


You were - ulikuwa / mlikuwa
They were - walikuwa
We were - tulikuwa
Asha and Asnat were - Asha na Asnat walikuwa

MIFANO :

I was going home.
(Nilikuwa naenda nyumbani.)

They were waiting for me.
(Walikuwa wananisubiria mimi.)


My mother was living here.
(Mama yangu alikuwa anaishi hapa.)

She was saying the truth.
(Alikuwa anasema ukweli.)

I was listening to radio.
(Nilikuwa nasikiliza radio.)

2. Sentensi za kukanusha

Muundo wa sentensi hizi huwa hivi:

Mtenda + was / were + not + verb + ing

You were not watching TV.
(Wewe ulikuwa huangalii TV.)

I was not listening to music.
(Mimi nilikuwa sisikilizi mziki.)

Zena was not reading a book.
(Zena alikuwa hasomi kitabu.)

We were not living here.
(Sisi hatuishi hapa.)3. Sentensi za kuuliza maswali

Muundo wa sentensi hizi huwa hivi:
was / were + mtenda + verb + ing
MIFANO :


Were you watching TV?
(Je ulikuwa unaangalia TV?)

What were you doing?
(Je ulikuwa unafanya nini?)

Was Anna reading a book?
(Je Anna alikuwa anasoma kitabu?)

Were they playing football?
(Je walikuwa wanacheza mpira?)


She was not saying the truth.
(Alikuwa hasemi ukweli.)

No comments:

Post a comment

Post Top Ad

UJUMBE MUHIMU KWA AJILI YAKO WEWE MSOMAJI:

"TUNAWASAIDIA WATU KUJIFUNZA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA KWA KUJIAMINI ZAIDI KUPITIA WHATSAPP"