Past Perfect
Continuous Tense nyakati hii inaelezea vitendo ambavyo vimefanyika
wakati uliopita katika hali timilifu ambayo ilikuwa ni ya kuendelea.
Mfano :
I had been
working.
(Nilikuwa
nimekuwa nikifanya kazi.)
Sasa tuangalie miundo au
jinsi ya kutengeneza sentensi katika nyakati hii,
MIUNDO YA
SENTENSI
Kama kawaida huwa tuna miundo
mitatu ya sentensi ambayo ni :
1. Sentensi za
kukubali / chanya
2. Sentensi za
kukanusha
3. Sentensi za
kuuliza maswali
1. Sentensi chanya
Mtenda + had + been + verb + ing
Examples
:
She had been cooking.
(Alikuwa amekuwa akifanya kazi.)
We had been playing
tennis.
(Tulikuwa tumekuwa tukicheza tenesi.)
Rama had been waiting
for two hours when I arrived.
(Rama alikuwa amekuwa akisubiri kwa masaa mawili nilipofika.)
They had been eating.
(Walikuwa wamekuwa wakila.)
We had been walking.
(Tulikuwa tumekuwa tukitembea.)
2. Sentensi za kukanusha
Muundo wa sentensi hizi huwa hivi:
Mtenda + had + not + been + verb + ing
Examples
:
It had not been
working well.
(haikuwa imekuwa ikifanya kazi
vizuri.)
I had not been reading my books.
(sikuwa nimekuwa nikisoma
vitabu vyangu.)
Sam and I had not been playing football.
(Mimi na Sam hatukuwa
tumekuwa tukicheza mpira.)
You had not been speaking English well.
(Wewe haukuwa ukiongea
kiingereza vizuri,)
Mary had not been watching Tv.
(Mary hakuwa amekuwa
akiiangalia Tv.)
3. Sentensi za kuuliza maswali
Had + mtenda + been + verb + ing
Mfano : Had you
been.......
Had you been drinking?
(Je ulikuwa umekuwa ukinywa?)
Had they been waiting long?
(Je walikuwa wamekuwa wamesubiri kwa muda mrefu?)
Had you been working here?
(Je! ulikuwa umekuwa ukifanya kazi hapa?)
Had they been starting?
(Je! Walikuwa wamekuwa wakianza?)
MIFANO ZAIDI
:
He had been taking
medicine for six months.
(Alikuwa amekuwa akitumia dawa
kwa miezi sita.)
They had not been doing
their work since 2003.
(Hawakuwa wamekuwa wakifanya kazi zao tangu 2003.)
I had not been listening
to music since Thursday.
(Sikuwa nimekuwa nikisikiliza
muziki tangu Alhamisi.)
Had you been helping your parents for two
years?
(Je! Ulikuwa umekuwa
ukiwasaidia wazazi wako kwa miaka miwili?)
Had the baby been crying?
(Je! Mtoto alikuwa amekuwa
analia?)
Had she been singing songs since 8 O'Clock?
(Alikuwa amekuwa akiimba nyimbo
tangu saa nane?
0 Comments