Simple Future Tense - English Kona

Hot

Post Top Ad


Wednesday, 16 September 2020

Simple Future Tense


Simple Future Tense hii nyakati ambayo tunaitumia kuongelea vitendo ambavyo vitafanyika wakati ujao. Ktika tense hii  verbs zetu huwa hazibadilik... zunakuwa katika hali yake ya asili (infinitive)


..................................

I will : Nita
You will : Uta
He/she / it : Ata
We will ; Tuta
They will : Wata

..................................

Rama will : Rama ata

James will : James ata

MIUNDO YA SENTENSI 

Kuna miundo  hii ambayo ni :

1. Sentensi za kukubali / chanya
2. Sentensi za kukanusha
3. Sentensi za kuuliza maswali


1. Sentensi chanya

Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :

Mtenda +  will + verb

Mifano ya sentensi

I will open the door.
(Nitafungua mlango)

My wife will buy a car.
(Mke wangu atanunua gari.)

I will go with you.
(Nitaenda na wewe.)

He will come here tomorrow
(Atakuja hapa kesho.) 

She will arrive on time.
(Atawasiri kwa wakati.)

Our cat will die.
(Paka wetu atakufa.)


2. Sentensi za kukanusha

Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :

Mtenda + will + not + verb

Mifano ya sentensi 

I will not open the door.
(sitafungua mlango.)

I will not go with you.
(Sitaenda na wewe.)

He will not come here tomorrow.
(Hatakuja hapa kesho.)

She will not arrive on time.
(Hatawasiri kwa wakati.)

Our cat will  not die.
(Paka wetu hatakufa.)


3. Sentensi za kuuliza maswali 

Muundo wa sentensi hizi unakuwa kama hivi :

Will + mtenda +  verb

 Mifano ya sentensi 

Will I open the door?
(Je nitafungua mlango?)

Will I go with you?
(Je nitaenda na wewe?

Will he come here tomorrow?
(Je atakuja hapa kesho?)

Will you eat my food?
(Je utakula chakula changu?)

Will she buy a new laptop at the end of this year ?
( Je atanunua laptop mpya mwisho wa mwaka huu ? )

{EnglishKona Tips

[Wakati mwengine huwa tunatumia SHALL badala ya WlILL lakini kwa nafsi ya kwanza umoja na wingi , yani I na WE  ]

 VIFUPISHO AMBAVYO TUNAVITUMIA KATIKA TENSE HII . 

I will  = I'll
You will = You'll
We will = We'll
He will = She'll
She will = She'll
They will = They'll

** ** **
I will not = I won't
You will not = You won't
He wil not = He won't
They will not = They won't


MIFANO ZAIDI :

Will you help me?
(Je! Utanisaidia?)

He won't help me.
(Yeye hatonisaidia.)

Nasra will buy a laptop at the end of this month.
(Nasra atanunua laptop mwisho wa mwezi huu.)

I'll start a new job.
(Nitaanza kazi mpya.)

I'll give you a nice gift.
(Nitakupa zawadi nzuri.)


No comments:

Post a comment

Post Top Ad

UJUMBE MUHIMU KWA AJILI YAKO WEWE MSOMAJI:

"TUNAWASAIDIA WATU KUJIFUNZA KUONGEA KIINGEREZA KWA UFASAHA NA KWA KUJIAMINI ZAIDI KUPITIA WHATSAPP"