Header Ads Widget

Njia 13 za kumsalimia mtu kwa Kiingereza

 


Tunahitaji kujua salamu tofauti tofauti katika Kiingereza ambazo zinatumika katika mazingira au hali tofauti tofauti.

Ni muhimu kujua njia tofauti tofauti ambazo watu husalimiana ili tuweze kuelewa watu wengine wanapotusalimia.

Kabla hatujaendelea tunapaswa kufahamu kwamba katika lugha ya kiingereza, kuna njia mbili za kuongea au kuwasiliana ambazo ni :

 

I. Formal English -  Kiingereza rasmi

II. Informal English - Kiingereza kisicho rasmi

 

Formal English (Kiingereza rasmi) – Hiki hutumika sana katika habari, biashara, kazini, serikalini,na kwa watu wanaoheshimiana, mfano mkubwa na mdogo, mtu na boss wake au kiongozi wake n.k

 

Informal English (Kiingereza kisicho rasmi) – Hiki hutumika katika mazingira ya kawaida katika maisha ya kila siku, mfano mtaani. 

Na hasahasa wazungumzaji wa asili (Waingereza na wamerakani) huwa wanafanya sana mazungumzo yao kwa njia hii wanapokuwa katika mazingira ya kawaida. Na hii ni hasahasa kwa watu wanaojuana na pia kwa wale ambao wapo katika rika moja.

Katika somo letu hili la leo tutajifunza salamu 13 ambazo utazitumia katika mazingira tofauti tofauti

Sasa tujifunze jinsi ya kusalimia kwa Kiingereza kwa njia zote hizi ,tuanze na Formal English (kiingereza rasmi.)

 

FORMAL ENGLISH – KIINGEREZA RASMI


1.   1.  Hello!

Tunatumia salamu muda wowote na katika hali yoyote ile. Na majibu ya salamu hii ni “Hello”. Hivyo mtu akikusalimia Hello na wewe unatakiwa kumjibu Hello!

 

2.     2.  Good morning – Habari ya asubuhi

Salamu hii inatumika asubuhi, na majibu ya salamu hii ni “Good morning”

 

 • A : Good morning
 • B : Good morning.

b)    

3.    3.  Good afternoon –  Habari ya mchana

Salamu hii inatumika mchana, na majibu ya salamu hii ni “Good afternoon”

 

 •     A : Good afternoon.
 •     B : Good afternoon.

 

4.     4.  Good evening –  Habari ya jioni

 Salamu hii inatumika jioni, na majibu ya salamu hii ni “Good evening”

 • A : Good evening. 
 • B : Good evening.

 

Note : “Good night” hii sio salamu, hii ni sawa na goodbye, yani unamuaga mtu kwa kumtakia usiku mwema. Hivyo ukikutana na mtu usiku usimsalimie kwa kumuambia good night, bali msalimie kwa kumuambia good evening, na mnapotaka kuagana ndo unamuamia “good night.”

 

5.     5. How are you? – Hujambo?

Tunaweza kuijibu kama hivi:

 

 •       I’m fine
 •       I’m good
 •       I’m okay

 

6.     6. Nice to meet you – Nimefurahi kukutana nawe.

Unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza, mkishasalimiana unaweza kumuambia “Nice to meet you” hapa ukiwa una maanisha umefurahi kukutana nae. Na jinsi ya kujibu hii unasema “Nice to meet you too” – Nimefurahi kukutana nawe pia.

 

 

7.     7. It’s pleasure to meet you = Nice to meet you

 Hii ni sawa tu na “Nice to meet you”

 

INFORMAL ENGLISH – KIINGEREZA KISICHO RASMI

 

Sasa tuangalie jinsi ya kusalimia kwa Kiingereza kwa kutumia Informal English unapokuwa katika mazingira  ya kawaida.

 

1.  Hi!

Hiki ni kifupi cha “Hello”. Unaweza kumsalimia mtu wakati wowote ule haijalishi mchana wala usiku. Na majibu ya salamu hii ni “Hi!”


2.  What’s up? – Vipi?

Salamu hii inatumika sana kwa marafiki. “What’s up?” inamuulizia mtu kama ana habari yoyote au kitu chochote special cha kuongeaa.

Na mara nyingi salamu hii hujibiwa kwa kusema “Nothing” Hii ina maanisha kuwa kila kitu kipo sawa na maisha yako yapo vizuri.

 

 • Ally : What’s up
 • Rose : Nothing. What’s up with you?
 • Ally  : Nothing new. Everything is good.

Lakini pia salamu inaweza kujibiwa kwa njia zingine. Hatuhitaji kujibu swali kwa sababu hii ni salamu tu na ambayo sio rasmi.

-         

 •    Halima : What’s up?
 •    Sharifu : Hey. How are you?  

 

 •   Halima : What’s up?
 •   Sharifu : I’m good. How are you?

  

3.  Sup?

Hii ni slang ya “What’s up?”. Na matumizi yake ni yaleyale tu yanafanana. Hii inatumika sana na vijana.

 

4.  How’s it going? – Inakuaje? 

Tunaweza kujibu salamu hii njia yoyote tunayotaka.

 

 •    A : How’s it going?
 •    B : Everything is going well. How about you?

 

 •    A : How’s it going?
 •    B : Everything is good.

 

 •    A : How’s it going?
 •    B :  I’m okay. How are you?

 

 •     A :   How’s it going?
 •     B :   Not well. I got fired yesterday. - Sio kwema. Nimefukuzwa kazi jana.


5.  How are you doing?  - Unaendeleaje? / hujambo?

Hii ni sawa na “How are you?”. Tunaweza kujibu salamu hii kwa kusema :

 

 •       I’m doing good
 •       I’m doing well.

 

Note : Hapa watu wengi wanachanganya na “What are you doing?”

 • What are you doing? = Unafanya nini?
 • How are you doing? = Hujambo? / Unaendeleaje?

Natumaini umeona tofauti hapo.


6.  How have you been? 

Swali hili linafanana na “How are you?”.

Hata hivyo “How are you?” inaulizia jinsi mtu anavyojisikia. Na “How have you been?” inamuulizia mtu kuhusu maisha yake kuanzia mara ya mwisho kuonana mpaka sasa.

 

Kwa mfano labda una rafiki yako hamajonana mwezi mzima, alafu siku mnakuja kuonana, basi utamuuliza “How have you been?” 

 

Tunaweza kujibu swali hili kwa njia yoyote tunayotaka, angalia hapa :

 •      I have been good.
 •      I’m good

 

7.  What’s new? – Kuna mpya gani?

Hii ni moja ya salamu ambayo inatumika sana miongoni mwa marafiki. Inaulizia tu kama kuna habari au kitu chochote kimetokea tangu mara ya mwisho kuonana.

Unaweza kujibu kwa kusema tu “Nothing” au kama ukitaka unaweza kuongea kitu chochote special ambacho kimekutokea hivi karibuni. 

Hapa tumefika mwisho wa somo letu la leo, tafadhali tufuatilie Facebook, Instagram na YouTube kwa jina la English Kona.

 

JIFUNZE KUONGEA KIINGEREZA  KWA UFASAHA KUPITIA WHATSAPP YAKO


Tunawasaidia watu kujifunza kuongea kiingereza kwa ufasaha kabisa.

Tunatoa kozi ya kiingereza kwa njia ya WhatsApp, ambayo mtu atasoma kwa njia ya Notes, Audio pamoja  Videos. 

Masomo yetu yapo katika mtiririko mzuri (kuanzia mwanzo mpaka mwisho).


Utapokea mafunzo yetu moja kwa moja kupitia  simu yako kila siku, yaan utakuwa unasoma wewe na mwalimu.


Na uzuri wa kozi yetu utajifunza mahali popote pale ulipo na muda wowote ule ambao utakuwa free.

Utafanya mazoezi ya kuongea ya kutosha, hivyo itakuwa rahisi kwako kuifahamu lugha hii kwa ufasaha zaidi.


Mafunzo yetu ni ya miezi minne mpaka kuwa fasaha.


Kwa sasa tupo katika OFA :

OFA YETU hii  ya leo ni utaweza kujiunga katika kozi yetu kwa gharama ya sh.7,000 tu mwezi mzima badala ya sh.15,000.

Hivyo ni wakati wako sasa wa kujifunza na kukiboresha kiingereza chako ili uweze kuongea kiingereza kwa ufasaha na kwa kujiamini zaidi.

 

JIUNGE leo kwa gharama ya sh.7,000 tu.

 

Bonyeza Hapa Kujiunga


 

Post a Comment

0 Comments