Mambo 7 Ambayo Unapaswa Kuyafahamu Ikiwa Unataka Kujifunza Kuongea Kiingereza Kwa Ufasaha Ndani Ya Muda Mchache (Hata Kama Hujui Kabisa Na Hata bila ya Kwenda Darasani)


Mambo 7 Ambayo Unapaswa Kuyafahamu Ikiwa Unataka Kujua Kuongea Kiingereza Kwa Ufasaha Ndani Ya Muda Mchache (Hata Kama Hujui Kabisa Na Hata bila ya Kwenda Darasani)


#1. Jifunze Phrases, na sio neno moja moja 


Ili uweze kuongea Kiingereza kwa ufasaha unatakiwa kujifunza Phrases (misemo) na wala sio neno moja moja.

 

Unapojifunza neno moja moja kinachotokea ni kwamba, pale unapotaka Kuongea unachukua muda mrefu sana kuunganisha neno moja moja (maneno) - Na mwisho wa siku unakuwa unaongea Kiingereza Kibovu.

 

Ila kama uki focus kwenye kujifunza phrases - basi utaweza kuongea Kiingereza kwa haraka.

 Mfano wa Phrases: 

1. I’m thirsty (Nina Kiu)

2. I’m hungry (Nina njaa.)

3. Don’t worry (Usijali)

4. I feel good. (Najisikia vizuri)

5. Wait a minute (Subiri kidogo.)

6. Ok then (Sawa basi)

7. Can you hear me? (Unanisikia?)

8. Are you afraid? (Unaogopa?)......N.k

 

Unapo focus kwenye kujifunza Phrases ambazo zinatumika kila siku, unakuwa una uwezo wa Kuongea Kiingereza kwa haraka na kwa ufasaha.

Unakuwa hauhitaji muda mwingi sana kufikiria nini cha kujibu au kuongea. Sentensi zako zinakuwa zinakamilika vizuri kabisa.


#2. Sikiliza sana Kiingereza Wanafunzi wengi wanaojifunza Kiingereza wanakuwa wanatumia muda wao mwingi sana kwenye kusoma, alafu wanatumia muda mdogo sana kwenye kusikiliza. 

 

Lakini mtoto mdogo anapojifunza lugha yake mama, anakuwa anaanza kusikiliza kwanza, kisha anaongea na baadae ndo anaanza kujifunza kuandika na kusoma.

 

Na hivi ndivyo inavyotakiwa katika Kiingereza, Unapaswa kusikiliza sana.

 

Kumbuka katika mazungumzo yoyote yale, asilimia 50 unakuwa unasikiliza na asilimia 50 unakuwa unaongea. Sasa kama unakuwa huelewi mtu mwingine anachoongea, Je utawezaje kumjibu? Hapana, hutoweza kumjibu.

 

Hivyo kama unataka kuongea Kiingereza kwa ufasaha, basi unatakiwa kufanya mazoezi ya kusikiliza sana Kiingereza.

 

Na pia unapokuwa unasikiliza zaidi, unakuwa unaboresha uwezo wako wa Kuongea Kiingereza kwa ufasaha automatically.

 

#3. Fanya mazoezi ya KuongeaIli uweze Kuongea Kiingereza unatakiwa kufanya mazoezi ya kuongea sana, hii inakusaidia kuwa fasaha katika lugha hii. Kama hujaribu kuongea basi hautaweza kuwa fasaha katika lugha hii.


#4. Jifunze Kufikiria katika Kiingereza


Je huwa una tabia ya kufikiria kwa Kiswahili alaf una tafsiri kwa Kiingereza kabla ya kuongea? Kama una tabia hiyo, USIFANYE TAFADHALI ..... 


Kwa sababu unakuwa unatengeneza sentensi ambazo haziko natural, na zenye makosa. Hii inatokana sarufi ya Kiswahili na Kiingereza haifanani (yaan mpangilio wa sentensi za Kiswahili haufanani na mpangilio wa sentensi za Kiingereza)


Hivyo mwishowe unakuwa unaongea Kiingereza kibovu. Na pia unakuwa unatumia muda mwingi wa kufikiria sana, na mwisho wa siku unakuwa unaongea kwa kusitasita na kukwama kwama.


Unachotakiwa kufanya ni kujifunza kufikiria kwa Kiingereza, hii itakufanya uweze Kuongea Kiingereza kwa Ufasaha.


#5. Usiogope kufanya makosa


Je huwa unapata hofu kuongea Kiingereza kwa sababu unaogopa kufanya makosa au kuongea Kiingereza kibovu?


Kama jibu ndio, basi kumbuka hili -  dhumuni la Kiingereza ni kuwasiliana. Japokuwa Grammar ni muhimu, lakini sio muhimu sana kuliko Mawasiliano katika Kuongea Kiingereza.

Ngoja nikuambie kitu ambacho huenda ukifahamu, hata wazungumzaji wa asili wa lugha hii huwa wanafanya makosa wakati wa mazungumzo, sasa we nani mpaka uogope kufanya makosa? Na uzuri unapofanya makosa unakuwa unajifunza ili wakati mwingine tena usirudie kosa hilo. Ila ukikaa kimya unakuwa hujifunzi chochote.


Ngoja nikupe mfano - kama ukisema ;


Yesterday I go to work


Ambayo ulikuwa una maana ya “Jana nilienda kazini.”


Sentensi hiyo haiko sawa kisarufi (grammatically), lakini bado inawasilisha ujumbe wako katika mawasiliano. 

Mzungumzaji wa Kiingereza atakuelewa una maanisha nini.


Hivyo ni bora kusema kitu ambacho sio sahihi ambacho bado ujumbe utafika vizuri, kuliko kukaa kimya kabisa ukashindwa kuwasiliana.


Kwahiyo usikae kimya, usiogope kufanya makosa.... Unapofanya makosa ndivyo unavyozidi kujifunza (ukiwa unaerekebishwa)


Hivyo weka akilini kuwa 𝐃𝐡𝐮𝐦𝐮𝐧𝐢 𝐥𝐚 𝐊𝐢𝐢𝐧𝐠𝐞𝐫𝐞𝐳𝐚 𝐧𝐢 𝐊𝐮𝐰𝐚𝐬𝐢𝐥𝐢𝐚𝐧𝐚.


#6. Ongea Polepole 


Kujaribu kuongea haraka haraka hakukufanyi kuonekana kama fundi wa Kiingereza. Badala yake itakuwa ngumu kwa watu kukuelewa unachokiongea.


Kuongea Kiingereza polepole kuna faida mbili;


• Inakupa muda zaidi kufikiria cha kusema

• Inamrahishia mtu kukuelewa kwa urahisi.


Na unavyozidi kufanya mazoezi, Kiingereza chako cha Kuongea kinazidi kuwa bora zaidi na haraka zaidi.


#7. Relax, kuwa na Mawazo chanya na Jiamini


Kama umefanya makosa au umesahau neno wakati unazungumza Kiingereza — Ni sawa Tu Usiwe na wasiwasi na wala usiogope.


Huyo mtu unayeongea nae atakuelewa tu unachomaanisha.
Lakini kama ikiwa unaogopa Kuongea Kiingereza eti kwa sababu unahofia kuchapia, basi itakuwa ngumu kwako kufanikiwa kujua Kuongea Kiingereza kwa ufasaha.


Hivyo usiseme “Kiingereza changu kibovu” - Haya mawazo hasi hayatakusaidia kabisa.


Hivyo badala yake, we fikiria tu ”I can speak English” Hii itakupa confidence na itakusaidia wewe kuongea vizuri.


Je ungependa tukushike mkono katika safari yako ya kujifunza Kiingereza mpaka kuwa fasaha katika lugha hii? Kama jibu lako ndiyo tunakukaribisha katika kozi yetu maalumu ya Kiingereza inayofanyika WhatsApp inayoitwa WhatsApp English Course.

Katika course hii tutakushika mkono, na tutakuwa na wewe bega kwa bega mpaka unakuwa fasaha ndani ya miezi minne tu (Hata kama hujui kabisa.) 

Kupitia course hii utajifunza kuongea Kiingereza kwa ufasaha na kwa Kujiamini zaidi.


Utapata mafunzo kwa mpangilio mzuri (kuanzia mwanzo mpaka mwisho)


Utasoma kwa njia ya notes, audio pamoja na video.


Unapokea mafunzo yetu moja kwa moja kupitia simu yako kila siku, yaan utakuwa unasoma wewe binafsi tu na sio kwenye group (hii itakuwa rahisi kwako kuelewa)


𝐘𝐚𝐧𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐤𝐢𝐟𝐮𝐩𝐢 𝐮𝐭𝐚𝐰𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐮𝐳𝐮𝐧𝐠𝐮𝐦𝐳𝐚 𝐊𝐢𝐢𝐧𝐠𝐞𝐫𝐞𝐳𝐚 𝐤𝐰𝐚 𝐔𝐟𝐚𝐬𝐚𝐡𝐚 𝐧𝐚 𝐊𝐮𝐣𝐢𝐚𝐦𝐢𝐧𝐢 𝐍𝐝𝐚𝐧𝐢 𝐲𝐚 𝐌𝐢𝐞𝐳𝐢 𝐌𝐢𝐧𝐧𝐞 𝐓𝐮


Njia yetu inakurahisishia wewe Kuongea Kiingereza Kwa Ufasaha na Kujiamini katika mazingira yoyote yale ya kila siku. Tutakupatia masomo ambayo ni bora kwako. Siyo marahisi sana na wala sio magumu sana.


Yani hata kama hujui kabisa, course hii ni kwa ajili yako itakusaidia kutoka 𝐙𝐞𝐫𝐨 mpaka kuwa 𝐇𝐞𝐫𝐨.


Naamini dhumuni lako kubwa mpaka umefika hapa ni kutaka kujua Kuongea Kiingereza Kwa Ufasaha.

Na Unastahili kufanikiwa juu ya hilo.


Uzuri wa kozi yetu utajifunza mahali popote pale ulipo na muda wowote ule ambao utakuwa free.


Katika kozi hiii utafanya mazoezi ya kuongea ya kutosha, hivyo itakuwa rahisi kwako kuifahamu lugha hii kwa urahisi zaidi.


Unapofanya makosa unaerekebishwa na kufutwa hayo makosa.


Muda Ni Sasa

Bonyeza Hapa Kujiunga


 

Post a Comment

0 Comments